English
Kuhusu Sisi
Malengo
Msaada
Fomu za Maombi
Darsah za Mwezi
Matangazo
Wasiliana Nasi
Michango & Misaada
Michango
Madrasatunnur

Madhumuni pekee ya Madrasatunnur Educational Trust ni kuhudumia Jamii, na tatizo liliopo kuwa hatuapati msaada wa aina yoyote wa kila tuitegemee jamii yenyewe yaani nikizungumza hivi ina maana ni (wewe).

Juu ya hivyo tutazidi kumshukuru Allah pamoja na wewe ikiwa utaweza msaada wa aina yoyote ambao umo ndani ya uwezo wako,lakini njia bora na njema kabisa ikiwa utaweza kutusaidia kwa kutoa msaada wa kifedha, ukihisi waweza kututsaidia kwa njia nyengine zaidi ya hiyo basi tafadhali tunakuomba wasiliana nasi kwa kutuandikia email kwenye anuani hii hapa

Sehemu nyengine ya kusomeshea

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukipata tabu katika sehemu ya kusomeshea vijana hadi watu wazima pale wanapokuja kutafuta elimu, sehemu tuliokodi inagharimu fedha nyingi na kama tulivyosema kuwa mara zote huwa tunategemea Sadaqah kutoka kwa jamii ili kuendeleza taasisi hii, na mchango mkubwa hutolewa na wazee wa wanafunzi. Kwa sasa kila mwaka tunalipa jumla ya £7000. kwa mwaka, na fedha hizo ni kwa ajali ya siku za Jumamosi na Jumapili tu kwa wiki, ni Jumla ya masaa 9, kwa siku zote mbili. (Jumamosi masaa 5 na Jumapili Masaa 4)

Kutokana na maombi mengi ya wazazi ya kutaka watoto wao kuja kupata elimu hapa kwenye madrasah, tunashindwa kuwapokea kutokana na sehemu tuliyokodi ni ndogo vile vile, kwa mujibu wa taratibu za afya na usalama ukumbi tulionao umeruhusiwa kuchukua watu wasiozidi 90, lakini hadi sasa tuna wanafunzi wasiopungua 176.

Ili tuweze kupata sehemu nyengine iliokuwa kubwa na iwe ya mali yetu kama Jamii, tumeanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya maradi huu ambao umeanza mwezi wa October 2009. Na tayari tumeshaanza kupokea michango kutoka kwa watu mbali mbali.

Shabaha yetu ni kukusanya jumla ya £700.000.00. Na Ishaallah tutafanikiwa na tunakuomba nawe pia ujiunge pamoja nasi kwenye jambo hili la kheri. na ukurasa huu utakuwa ukiwajuulisha Ummah jumla ya mapato yaliopatikana kila mwezi Inshaallah. (Hadi mwisho wa Mwezi wa October tumeshakusanya £1170.00)

TUNAHITAJI MSAADA WAKO SASA

Unaweza kufanya malipo moja kwa moja kwenye Account ya Madrasah

Islamic Bank of Britain
Madrasatunnur Educational Trust
A/C No: 01158850
S/C No: 30-00-83


Ama waweza kutoa mchango wako kwa kutumia PAYPAL

Vile vile tunakuomba kama wewe ni mkaazi wa UK na mlipa kodi (Tax), Tafadhali tunakuomba Dowload fomu unayoitwa Gift Aid, ijaze fomu hiyo kisha turejeshee.kwani fomu hiyo ukijaza itawezekana kupata ongezeko la asimilia 28% ya mchango wako kutoka Inland Revenue

Download: Gift Aid Form & Standing order mandate

Madrasatunnur Educational Trust