|
Utangulizi
Madrasatunnur Educational Trust ni Taasisi ya
Elimu ya mafunzo ya Kiislam, Taasisi hii imefunguliwa kutokana na
kuonekana upo umuhimu wa kuwa nayo sisi watu wa mwambao wa Africa
Mashariki ambao tunaishi UK. Taasisi ipo katika Mji wa Southall
Kwenye ukumbi wa Convent Way Community Hall ndani ya London Borough
of Hounslow, na imepata usajili wa kudumu Tarehe 23 December 2003
kutoka kwa msajili wa UK Charity Commission. na Nambari yake ya
Usajili ni
1101074.
Kwa sasa Madrasah inatoa huduma za mafunzo ya
Elimu ya Quran, Sira, Hadith, Tarbiyyah, Akhlaq na mengi mengineyo.
Hadi sasa Madrasah ina wanafunzi zaidi ya 180 na ina walimu wa
kujitolea 10, na Inshaallah tupo tayari kupokea wengine ikiwa
watajitokeza katika mradi huu, kwani wengi wetu tunafahamu umuhimu
wa elimu.
Lengo Letu
Madrasah ni kutoa huduma za elimu kwa watoto kuanzia Umri wa Miaka 5 hadi 20, kwenye siku za Jumamosi na Jumapili kuanzia saa Nne asubuhi hadi saa Tisa mchana kwa siku za Jumamosi na siku za Jumapili hutoa huduma kuanzia saa Nne asubuhi hadi saa Nane mchana. Na Pia sasa tayari imefanikiwa kuanzisha masomo kwa watu wazima mwezi mara mbili kwa siku za Jumamosi.
Shabaha Yetu
Kufanya kazi kwa uzuri na Pamoja, kama Uislamu unavyo tufundisha. Kufanyakazi kwa pamoja ili kunyanyua ari ya ummah na kuwa elimisha hususan vijana wajibu wao katika dini, maisha yao na akhera yao. pia ni kuwatia ari vijana waweze kuzitenda na kuzifamu vyema thamani na maadili mema ya kiislamu kuanzia majumbani mwao na katika ngazi za kijamii na hata kitaifa kwa ujumla. pia lengo letu ni kuwatanabahisha mambo ya kiislamu kwa ujumla ili waweze kuwa na imani na kujiamini vya kutosha. Na kujenga matumaini ya Imani miongoni mwa Waislamu kwa ujumla.
|