Madrasatunnur Educational
Trust ni Taasisi ya Elimu ya mafunzo ya
Kiislam, Taasisi hii imefunguliwa kutokana
na kuonekana upo umuhimu wa kuwa nayo sisi
watu wa mwambao wa Africa Mashariki ambao
tunaishi UK.
Taasisi ipo katika Mji wa
Southall Kwenye ukumbi wa Convent Way
Community Hall ndani ya London Borough of
Hounslow, na imepata usajili wa kudumu
Tarehe 23 December 2003 kutoka kwa msajili
wa UK Charity Commission. na Nambari yake ya
Usajili ni
1101074.
Kwa sasa Madrasah inatoa
huduma za mafunzo ya Elimu ya Quran, Sira,
Hadith, Tarbiyyah, Akhlaq na mengi mengineyo.
Hadi sasa Madrasah ina wanafunzi zaidi ya
180 na ina walimu wa kujitolea 10, na
Inshaallah tupo tayari kupokea wengine ikiwa
watajitokeza katika mradi huu, kwani wengi
wetu tunafahamu umuhimu wa elimu.
Lengo Letu.
Madrasah ni kutoa huduma za
elimu kwa watoto kuanzia Umri wa Miaka 5
hadi 16, kwenye siku za Jumamosi na Jumapili
kuanzia saa Nne asubuhi hadi saa Tisa mchana
kwa siku za Jumamosi na siku za Jumapili
hutoa huduma kuanzia saa Nne asubuhi hadi
saa Nane mchana. Na Pia sasa tayari
imefanikiwa kuanzisha masomo kwa watu wazima
mwezi mara mbili kwa siku za Jumamosi.
Shabaha Yetu
Kufanya kazi kwa uzuri na
Pamoja, kama Uislamu unavyo tufundisha.
Kufanyakazi kwa pamoja ili kunyanyua ari ya
ummah na kuwa elimisha hususan vijana wajibu
wao katika dini, maisha yao na akhera yao.
pia ni kuwatia ari vijana waweze kuzitenda
na kuzifamu vyema thamani na maadili mema ya
kiislamu kuanzia majumbani mwao na katika
ngazi za kijamii na hata kitaifa kwa ujumla.
pia lengo letu ni kuwatanabahisha mambo ya
kiislamu kwa ujumla ili waweze kuwa na imani
na kujiamini vya kutosha. Na kujenga
matumaini ya Imani miongoni mwa Waislamu kwa
ujumla.
|